fbpx OMEGA - agiza teksi
Jisajili kama dereva

Chagua njia rahisi ya usajili:

kabidhi Maombi yako

  Andika "Dereva" kwa njia yoyote ya meseji kwenye mitandao ya kijamii au kabidhi Maombi yako kupitia fomu na mtaalamu wetu atakutafuta.

  Maswali yanayoulizwa mara Kwa mara

  Unahitaji gari lenye hali nzuri na simu mahiri (Smartphone) iliyo mtandaoni. Katika dakika chache, utaweza kujisajili tovutini. Ikiwa una maswali yoyote, unaweza kuwasiliana nasi kwa kubonyeza sehemu ya mawasiliano.
  Tunahimiza ufuate sheria za trafiki. Tunashauri uliweke gari lako katika hali nzuri, hakikisha kuwa nafasi ya abiria ni safi. Gari lapaswa kuwa na mafuta kila kila mara. Dereva anapaswa awe na heshima, mwenye tabia njema na anayeweza kutatua migogoro itakayotokea. Kwa mfano, ni vyema kuwakumbusha abiria wasisahau vitu vyao garini mwishoni mwa safari.
  Programu inaitwa Taxsee Driver na inapatika kwenye Google Play Store na App Store. Programu imepakuliwa na watu zaidi ya milioni tatu kwenye mfumo wa Android. Hii ni rekodi kubwa miongoni mwa kampunia za teksi Urusini. Unaweza kuipata kwa kutafuta neno "Taxsee Driver".
  Maagizo yote ya teksi yanapatikana kwa programu kwenye orodha ya jumla iliyogawanywa kwa makundi. Unaweza kuona maagizo yaliyo kwenye jamii ya miji/'city' au kwenye jamii ya umbali/'long distance'. Unaweza kuchagua agizo lililokaribu nawe au muda maalum. Utapata maagizo ya gari baada ya abiria kuagiza gari. Tunahimiza utumizi wa 'automatic'/mfumo unaojiendesha kwa kuwa huo ndio rahisi kutumia.
  Ndio. Dereva anaweza timiza maagizo wakati unaomfaa tu iwe jioni au hata usiku. Dereva anaweza kutimiza maagizo anapoenda kazini. Dereva ndiye mwenye kuchagua ratiba yake na pesa anazopata, akiamua kupumzika, ni sawa kwa kuwa mapumziko ni mazuri kwa afya binafsi na kwa kudumisha ubora wa huduma.
  Nauli inaamuliwa na vigezo vingi : bei ya mafuta ya gari, gharama za ukarabati na matengenezo ya gari na bima. Nauli pia inaamuliwa na ugavi na uhitaji wa magari, ushindani na makampuni mengine na ushuru katika kila jiji. Huduma hii inajaribu kusawazisha maslahi ya washiriki (madereva na abiria).
  Mapato mengi huwa wakati wa hali mbaya ya hewa, sikukuu na sherehe. Asubuhi na jioni watu wanapoenda kazi na kurudi nyumbani ni wakati mzuri sana wa kuzidisha pesa unazopata. Abiria wanaopata huduma nzuri hupeana vidokeo (tips), kwa mfano, magari yanayowasili haraka. Dereva anapwaswa kupeana huduma bora ili apate maoni chanya. Madereva wenye gari zenye vibandiko vyenye matangazo ya Taxsee watapewa kipaumbele kupata abiria.

  kabidhi Maombi yako